the download will begin in 10 seconds (limit : 500ko/s)
1. بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ
1. Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mjawa wa rehema, Mrehemevu.
2. ٱلۡحَمۡدُ لِلَّهِ رَبِّ ٱلۡعَٰلَمِينَ
2. Sifa njema ni za Mwenyezi Mungu, Mola wa walimwengu.
3. ٱلرَّحۡمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ
3. Mjawa wa rehema, Mrehemevu.
4. مَٰلِكِ يَوۡمِ ٱلدِّينِ
4. Mwenye kumiliki Siku ya Malipo.
5. إِيَّاكَ نَعۡبُدُ وَإِيَّاكَ نَسۡتَعِينُ
5. Wewe tu tunakuabudu, na Wewe tu tunakuomba msaada.
6. ٱهۡدِنَا ٱلصِّرَٰطَ ٱلۡمُسۡتَقِيمَ
6. Tuongoze kwenye njia nyofu.
7. صِرَٰطَ ٱلَّذِينَ أَنۡعَمۡتَ عَلَيۡهِمۡ غَيۡرِ ٱلۡمَغۡضُوبِ عَلَيۡهِمۡ وَلَا ٱلضَّآلِّينَ
7. Njia ya wale uliowaneemesha, siyo ya waliokasirikiwa, wala ya waliopotea.